Skip to main content
Skip to main content

Nauli zapanda maradufu kufuatia kupanda kwa bei ya mafuta

  • | Citizen TV
    5,085 views
    Duration: 3:43
    Kupanda maradufu kwa bei ya mafuta nchini kumewatosa wamiliki wa magari ya uchukuzi na abiria kote nchini kwenye mafadhaiko zaidi. Punde tu baada ya bei mpya kuanza kutekelezwa saa sita usiku, wadau katika sekta ya usafiri walijibu kwa kupandisha nauli za usafiri, huku gharama zaidi zikitarajiwa kadri wahudumu wanavyoendelea kutathmini ongezeko la gharama za utoaji huduma . Na kama anavyoarifu ben kirui, katika vituo vikuu vya basi, abiria walipigwa na butwaa kutokana na ongezeko la nauli lililoanza kutekelezwa mara moja.