- 2,679 viewsDuration: 50sChama cha uda kimepuuzilia mbali uamuzi wa mahakama kuu wa hapo jana ulioharamisha ndoa ya chama cha uda na anc, naibu kinara wa chama cha uda gavana wa lamu issa timamy, akisema mahakama ilikosea kutoa uamuzi huo. Timamy anasema chama cha anc kilivunjwa kulingana na sheria na kuwa chama hicho hakipo kwa sasa. Anc ilivunjwa rasmi januari mwaka uliopita, baadhi ya viongozi wake wakijiunga na chama cha rais william ruto cha uda. Issa timamy aliyekuwa kinara wa chama cha anc aliteuliwa naibu kinara wa pili wa uda.