Huku zoezi la kuwasajili wanafunzi wa gredi ya 10 likiingia siku ya mwisho hii leo, wanafunzi wawili kutoka familia moja kule Kijiwetanga, Malindi kaunti ya Kilifi huenda wakakosa nafasi hiyo kwa kukosa uwezo wa kifedha.
Lucy Mwalimu na Stephen Mwalimu, wanafunzi waliofanya mtihani wa gredi ya 9 katika shule ya msingi ya Kijiwetanga wanasema mama yao hana uwezo wa kulipa karo pamoja na kununua bidhaa mbali mbali zinazohitajika baada yao kuitwa katika shule za Moi Forces Mombasa na St George's Kaloleni . Baba ya watoto hao alifungwa jela miaka minne iliyopita. Wawili hao sasa wanawaomba wahisani kujitokeza na kuwasaidia ili waweze kuendeleza masomo yao na hatimaye kusaidia familia yao.