Huku ikiwa imesalia mwezi mmoja kabla ya chaguzi ndogo katika eneo bunge la Isiolo south na wadi za west Kabras, Muminji na Evurore, chama cha National Economic Development kimezindua wagombea wake watakaowania viti hivyo.
Isaac Abduba fayo atapeperusha bendera ya chama huko Isiolo kusini, George Musini mukhwana ameteuliwa kuwania kiti cha mwakilishi wadi west Kabras huku Cosmas Njeru na Martin Mukundi wakikabidhiwa tiketi za kuwania wadi za muminji na evurore kule mbeere kaskazini. Kinara wa chama hicho Mike Sonko amesema licha ya kuwa ni chama kipya ambacho kinajitosa kwenye uchaguzi kwa mara ya kwanza, wameweka mikakati dhabiti kuhakikisha wanashinda viti hivyo na kuandikisha historia.