- 2,451 viewsDuration: 3:34Wiki mbili zilizopita, kada wa CCM mkoani Tanga Kazungu Bakari Kazungu alivamiwa nyumbani kwake na watu waliogoma kujitambulisha. Kazungu ameiambia BBC Swahili kwamba watu hao walimchukua kwa nguvu, wakamfunga pingu, kumpandisha kwenye gari, kumfunga kitambaa cheusi kichwani na kuzunguka nae kwa muda mrefu huku wakimuhoji na kumpiga kila mara alipotoa majibu wasiyoridhika nayo. Kuhusu tukio la kutekwa kwa Kazungu, Polisi Mkoa wa Tanga wamethibitisha kutokea, na kumuhoji Kazungu na kwamba uchunguzi wa kina wa tukio hilo unaendelea.Hata hivyo BBC pia ilimtafuta kiongozi wa polisi mkoani Tanga lakini hakupatikana na wala kujibu ujumbe. Yafuatayo ni sehemu ya mazungumzo kati ya Kazungu na mwandishi wa BBC @sammyawami kwa njia ya simu. - - #bbcswahili #siasa #utekaji Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw