- 336 viewsDuration: 3:02Wagonjwa wanao hitaji huduma za dharura katika hospitali ya rufaa ya samburu, wakiwemo watoto njiti wamepata afueni, kufuatia uzinduzi wa mradi wa nishati ya jua katika hospitali hiyo. Hii Ni mojawapo ya mikakati ya kuboresha huduma za matibabu kwenye hospitali hiyo ya rufaa, hii ni kufuatia tatizo la kupotea kwa nguvu za umeme kila mara hatua ambayo hutatiza huduma za matibabu.