Skip to main content
Skip to main content

Pesa za inua Jamii

  • | Citizen TV
    177 views
    Duration: 1:57
    Wakazi wa kaunti ndogo ya Manga katika kaunti ya Nyamira wamelalamikia changamoto zinazotatiza usambazaji wa pesa za inua jamii kwa wazee, mayatima na walemavu kaunti hiyo. Wakizungumza kwenye hafla ya kusambaza vyakula na bidhaa zingine kwa wazee katika eneo hilo, mwakilishi wa kike wa kaunti ya Nyamira, Jerusha Momanyi na Kamishna wa Manga, Valentine Cherono, wameomba idara husika kushughulika na kutatua changamoto hizo kwa haraka. Baadhi ya wakazi wamedai kutopokea pesa hizo kwa zaidi ya miezi minne sasa, huku baadhi wakikosa kupokea mara kwa mara.