Picha za angani zaonesha athari za mafuriko maeneo mengi

  • | Citizen TV
    11,501 views

    Jumla ya familia 250 ambazo zimelazimika kuhama kwao kutokana na kufurika kwa bwawa la Masinga wanaishi kambini bila msaada wowote. Aidha, shughuli za uchukuzi zimesitishwa katika maeneo ya Athi River, Ruiru na Oldonyo Sabuk, ambako pia mafuriko yamesomba makazi na mimea mashambani. Seth Olale aliruka angani kwa ndege kutazama kwa kina athari ya mafuriko.