Skip to main content
Skip to main content

Polisi mpakani Namanga wamewakamata washukiwa wawili wakisafirisha bangi

  • | Citizen TV
    1,153 views
    Duration: 2:12
    Maafisa wa polisi kutoka mpakani Namanga, Kaunti ya Kajiado, wamewakamata washukiwa wawili na kunasa bangi ya thamani ya shilingi milioni 2.5 iliyokuwa ikisafirishwa kuelekea jijini Nairobi... Bangi hiyo, ilikuwa imefichwa kama mizigo ya kawaida ndani ya basi moja lililokuwa likisafiri kutoka Dar es Salaam, Tanzania, kuelekea Nairobi. Bangi iligunduliwa wakati wa ukaguzi wa mizigo mpakani baada ya maafisa wa forodha, kwa ushirikiano na polisi wa Kenya, kukagua kwa makini mizigo iliyozua shaka. Washukiwa wawili wamekamatwa na kuzuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Namanga wakisubiri kufikishwa mahakamani. Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Kajiado, Alex Shikondi, amesemawanamsaka mshukiwa mkuu anayedaiwa kuwa alikuwa akisubiri mzigo huo jijini Nairobi.