- 1,032 viewsDuration: 4:08Rais William Ruto anapinga kile anachosema ni vichwa vya habari vinavyopotosha kufuatia kutolewa kwa Ripoti ya uchumi ya mwaka 2026 na shirika la Takwimu nchini KNBS. Takwimu mpya zinaonyesha kuwa kwa mwaka wa pili mfululizo ukuaji wa uchumi umepungua, kutoka asilimia 4.7 mwaka 2024 hadi asilimia 4.6 mwaka 2025. Ingawa takwimu zinaonyesha kushuka kidogo kwa kiwango cha ukuaji, Rais anasisitiza kuwa taswira halisi inaonyesha uthabiti, uundaji wa nafasi za ajira, na uthabiti wa uchumi kwa ujumla.