- 32,022 viewsDuration: 3:40Siku mbili baada ya watu 17 kufariki katika eneo la Mlima Kiu, Salama, kaunti ya Makueni, kwenye barabara kuu ya Nairobi-Mombasa, mwanahabari wetu Serfine Ouma alisafiri kutoka Nairobi hadi Salama. Lengo lilikuwa kukupa taswira halisi ya kile kinachochangia ajali kushuhudiwa mara kwa mara katika eneo hilo, na kubaini ni kwa nini Salama, licha ya jina lake, limegeuka kuwa ngome ya mauti.