Kaunti ya Nyandarua imezindua rasmi mpango wa lishe katika shule za Chekechea (ECDE) unaolenga kuimarisha masomo na kuboresha ustawi wa watoto wadogo.
Mpango huo uliozinduliwa katika Shule ya Mumbi Comprehensive katika Wadi ya Kaimbaga unanuia kuhakikisha watoto wanasalia shuleni mbali na kuboresha lishekwa watoto wadogo. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Gavana Moses Kiarie Badilisha alisema mpango huo utawafaidi maelfu ya watoto katika kaunti nzima, huku serikali kwa sasa ikijenga zaidi ya majiko 25 ya kisasa ambayo yanatarajiwa kuhudumia zaidi ya wanafunzi 24,000.