Shisha si haramu | Wafanyibiashara na wavutaji shisha wapata afueni

  • | Citizen TV
    3,008 views

    Juhudi za kukomesha biashara na uvutaji shisha nchini zimepata pigo baada ya mahakama ya shanzu kuamua kuwa hakuna sheria yoyote nchini inayoharamisha shisha. Hakimu Mwandamizi Joe Omido amesema kuwa marufuku inayotajwa na serikali na Nacada haina msingi wowote kisheria kwani wizara ya afya haikuchukua hatua zilizohitajika kuwasilisha mswada bungeni ili uidhinishwe kuwa sheria kama iliyoagizwa na mahakama mwaka wa 2018. Uamuzi huo ulimfanya hakimu Omido kuwaachilia huru washukiwa 48 waliokamatwa kwa kufanya biashara au kuvuta shisha