Shughuli za kuwatafuta watu watatu ambao haijulikani waliko baada ya mashua kuzama huko Tudor kaunti ya Mombasa wakati wa hafla ya mchezo wa majini zimeshika kasi. Wakati wa mkasa huo, watu 19 waliokolewa huku watatu waliosalia wakiwa haijulikani waliko baada ya mashua walimokuwa kuzama jana jioni. Kundi la mashirika mbalimbali limekuwa likiwatafuta kwenye bahari hindi leo, ila halijafanikiwa, huku familia za waliopotea zikiwa na matumaini kwamba jamaa zao watapatikana wakiwa hai.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive