Skip to main content
Skip to main content

Shughuli za matibabu zimetatizika kwa muda Ilbisil Kajiado kutokana na mzozo wa Ambulensi

  • | Citizen TV
    44 views
    Shughuli za matibabu zimetatizika kwa muda katika Kituo cha Afya cha Ilbisil, Kaunti ya Kajiado, kufuatia maandamano ya wakazi waliokuwa wakipinga kuhamishwa kwa ambulensi kutoka kituo hicho hadi Hospitali ya Meto. Wakazi hao wanasema kuwa kuondolewa kwa ambulensi kumewaacha bila huduma muhimu ya dharura, hasa kwa kuwa kituo hicho kinahudumia idadi kubwa ya watu mashinani.Kwa mujibu wa wakazi, wagonjwa wanaopewa rufaa kwenda hospitali ya rufaa ya Kajiado hukumbwa na changamoto ya usafiri, hali inayowalazimu kutumia magari ya umma au binafsi. Wakazi pia wanasema kuwa akina mama wajawazito na watoto ndio wanaoathirika zaidi.