Baadhi ya viongozi wa chama cha Walimu wa Shule za Sekondari na Vyuo KUPPET tawi la Nandi, wamekosoa vikali Katiba ya sasa ya muungano huo ya mwaka 2024, wakisema inawabagua wanachama kutoka matawi madogo nchini kwa kuwanyima fursa ya kushika nyadhifa za kitaifa.
Wakizungumza eneo la Chepkumia kaunti ya Nandi, viongozi hao, walisema kuwa baadhi ya vipengele vya katiba hiyo vinatoa mapendeleo kwa matawi makubwa huku vikinyima matawi madogo fursa ya uongozi wa kitaifa. Katibu wa KUPPET, Nandi Paul Rotich alilalamikia gharama kubwa ya ada ya uteuzi kwa wanaowania nyadhifa za kitaifa, akisema kiwango hicho ni cha juu kuliko kile kinacholipwa na wagombea wa ubunge nchini.