Tume ya EACC yaasema ufisadi umekithiri kwenye utoaji zabuni

  • | Citizen TV
    199 views

    Tume ya kupambana na ufisadi nchini imedai kuwa asilimia 80 ya visa vya ufisadi nchini vinachangiwa na maafisa wa utoaji zabuni na ununuzi wa bidhaa serikalini. Akizungumza kwenye kongamano la siku tano linalowahusisha maafisa wa utoaji zabuni wa serikali kuu na za kaunti, naibu afisa mkuu wa tume ya EACC Abdul Mohamud amepinga pendekezo la kufanyiwa marekebisho mswada kuhusu vita dhidi ya ufisadi akisema hatua hiyo italemaza juhudi za kukabiliana na ufisadi nchini. Aidha tume hiyo inachunguza utoaji wa zabuni ya kemsa pamoja na serikali ya kaunti ya siaya ambapo zaidi ya shilingi bilioni moja zinadaiwa kufujwa.