Skip to main content
Skip to main content

Ubishi wa barabara Kilifi

  • | Citizen TV
    1,985 views
    Duration: 2:16
    Wakazi wa Mariakani kaunti ya Kilifi wameandamana hadi katika afisi za kampuni ya ujenzi wa barabara kuu ya Mombasa -Nairobi wakilalamikia kutohusishwa katika ujenzi wa barabara ya kutoka Mombasa hadi Mariakani. Wakazi hao wamesema kuwa kampuni ya inayojenga barabara hiyo imekataa kutoa mchoro wa barabara wanayoijenga na kufanya vikao vya umma kama inavyohitajika kisheria. Aidha wanadai kuna njama ya kuhamisha mradi wa jamii wa kituo cha kuegesha Malori hadi eneo lingine wakiitaka serikali ya kaunti ya Kilifi kutenga nafasi ya kutekeleza mradi huo katika eneo la Mariakani. Wakaazi hao sasa wametoa makataa ya siku saba kwa usimamizi wa kampuni hiyo kuwapatia majibu.