Ufahamu Msikiti Mkuu wa Makka: Moyo wa imani ya Kiislamu

  • | BBC Swahili
    1,174 views
    Msikiti Mkuu wa Makka ni mahali patakatifu sana kwa Waislamu duniani, ambapo mamilioni ya waumini hukusanyika kila mwaka kwa ajili ya ibada ya Hajj. Kwenye msikiti huu kuna Kaaba, jengo la mawe lenye umbo la mche mraba ambalo Waislamu wanaamini lilijengwa na Mitume Ibrahim na mwanawe Ismail, na ndiyo mwelekeo wa sala za Waislamu wote duniani. Msikiti huu umeendelea kupanuka kwa karne nyingi ili kuhimili idadi kubwa ya watu wanaokuja kusali, hasa wakati wa Hajj na Ramadhani. Leo unachukua eneo kubwa sana na unaweza kupokea hadi watu milioni tatu kwa siku, ukiwa umeboreshwa kwa vifaa vya kisasa kama viyoyozi, ngazi za umeme, na kamera za usalama, na hivyo kuendelea kuwa kitovu cha imani na umoja wa Waislamu duniani. Mwandishi wa BBC @munie_noor anauangazia msikiti huu maarufu 🎥: Frank Mavura - #bbcswahili #Hajj #IDD Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw