Serikali imehimizwa kuwapa watu wanaoshi na ulemavu (PWDs) nafasi za kazi na zabuni ili kujikimu kuichumi na kuboresha Maisha Yao. Wakisungumza mjini Nanyuki, Kaunti ya Laikipia, walitoa wito kwa Serikali pia kuanzisha mikakati ya kuwasaidia walezi wa watoto wanaoishi na ulemavu kwa kuongeza mitaji ya biashara na mgao wa zabuni kutoka Serikaliza za kaunti, Kwani wangu wao wana majukumu mengi na hushindwa kukidhi mahitaji ya familia zao. kulingana na David Ndung’u , Afisa msaidizi wa Mradi wa Light for the world na ambao huwazaidia watu wanaoishi na Ulemavu kaunti ya Laikipia , alibaini Kuwa licha ya matakwa ya kisheria , kaunti Nyingi bado zinatoa chini ya asilimia Moja ya zabuni kwa watu wenye ulemavu badala ya asilimia tano inayotakiwa kisheria. Kwa mujibu wa takwimu za kuhesabu watu inchini, takriban milioni 0.9 ni watu wenye ulemavu . Ujumuishaji wao kiuchumi unabaki Kuwa nguzo muhimu katika kufikia ukuaji wa haki wa kitaifa