Ukraine - Urusi: Meli kubwa ya kifahari ya Urusi yapigwa mnada huko Gibraltar

  • | BBC Swahili
    1,100 views
    Meli ya kifahari yenye thamani ya dola milioni 75 imepigwa mnada huko huko Gibraltar, eneo la Uingereza lililopo kusini mwa pwani ya Uhispania. Meli hiyo inadhaniwa kuwa ya kwanza kupigwa mnada kwa umma tangu Urusi iliposhambulia Ukraine. Meli kadhaa zinazohusishwa na Urusi zimeshikiliwa katika mataifa tofauti tofauti ulimwenguni kutokana na uvamizi wa Urusi kwa Ukraine. #bbcswahili #ukraine #urusi