Ukraine yaishambulia Urusi kwa ndege zisizo na rubani

  • | BBC Swahili
    4,448 views
    Ukraine imefanya shambulizi kubwa zaidi la ndege zisizo na rubani kwenye mji mkuu wa Urusi, huku ndege hizo zisizopungua 90 zikilenga Moscow. Takriban watu 3 waliuawa na wengine 17 kujeruhiwa. Kwa jumla, mikoa tisa ya Urusi ilishambuliwa, huku zaidi ya ndege zisizo na rubani 330 za Ukraine zikiharibiwa au kuzuiliwa, kulingana na Wizara ya Ulinzi ya Urusi. Mashambulizi haya yanajiri baada ya siku kadhaa za mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za Urusi nchini Ukraine.