Viongozi katika Kaunti ya Kajiado wanalalmika kufuatia kiwango cha chini cha wanafunzi wanaojiunga Na gredi ya 10 huku muda wa mwisho wa kuripoti shuleni uliowekwa na Wizara ya Elimu ukikamilika leo.
Viongozi hao wanasema wanafunzi wengi bado hawajaripoti katika shule walizoitwa, huku wazazi wakitaja umbali wa shule, upangaji usio sahihi wa shule, na ukosefu wa karo kuwa vikwazo vikuu vinavyoathiri elimu. Wazazi pia wamekosoa agizo la serikali linalowataka machifu kuwatafuta wanafunzi ambao hawajaripoti shuleni, wakisema ingekuwa bora zaidi kwa serikali kutoa suluhu kwa changamoto za kimsingi katika mfumo wa elimu.