- 6,491 viewsDuration: 7:20Rais wa Marekani Donald Trump ametia saini amri ya kuondoa Marekani katika mashirika 66 ya kimataifa - na karibia nusu ya mashirika hayo ni ya Umoja wa Mataifa. Ikulu ya Whitehouse imesema kuwa mashirika hayo yanafanya kazi kinyume na maslahi ya Washington. Mengi ya mashirika hayo hupambana na mabadiliko ya tabianchi na juhudi za kudumisha amani na demokrasia. Marekani pia imesitisha misaada yote kwa serikali ya Somalia, ikidai maafisa waliharibu ghala la Shirika la Chakula Duniani la Umoja wa Mataifa WFP, na kushikilia tani 76 za chakula cha msaada. #Trump #Somalia #WFP #Somalia #bbcswahili #bbcswahilileo #dirayaduniatv #bbcswahilidirayadunia #bbcswahilihabalileo Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw