Utafiti waonyesha wanawake wengi wameathiriwa kichocho cha kizazi

  • | Citizen TV
    98 views

    Washikadau katika sekta ya afya kaunti ya Kwale wanapendekeza kujumuishwa kwa ugonjwa wa kichochho cha uzazi kwa wanawake kwenye taratibu za kuthibiti na kutibu magonjwa ya afya ya uzazi. Hii ni kufuatia ripoti iliotolewa na kituo cha afya cha LVCT Health baada ya kufanya utafiti wa miaka miwili na nusu ulioonyesha kuwa ugonjwa huo uliotelekezwa na kutorekodiwa kwenye vituo vya afya unaathiri wanawake wengi.