Skip to main content
Skip to main content

Utamaduni wa Kaskazini wang’ara katika Madaraka Dei Wajir

  • | Citizen TV
    702 views
    Kwa mara ya kwanza katika historia ya Kenya, sherehe za kitaifa zimefanyika Kaskazini mwa nchi huku Kaunti ya Wajir ikiandaa maadhimisho ya mwaka huu ya Madaraka Dei. Mbali na hotuba na shughuli rasmi za serikali, hafla hiyo iliwapa Wakenya fursa ya kipekee kushuhudia utamaduni, mila na desturi za jamii za eneo hilo. Kuanzia ngoma za kitamaduni, mavazi ya asili na maonyesho mbalimbali ya kitamaduni, sherehe hizo zilidhihirisha urithi wa kipekee wa wakazi wa Kaskazini mwa Kenya. Tukio lililogusa wengi zaidi ni zawadi ya ngamia 100 kwa Rais William Ruto, ishara ya heshima na ukarimu unaothaminiwa katika jamii za eneo hilo. Mary Muoki anatuletea taswira ya shamrashamra zilizopamba siku hiyo ya kihistoria.