- 13,100 viewsDuration: 1:38Kwa miaka 16 Abdallah Bakari Sijambo maarufu kama @mhasibuwadaladalatz amekuwa kivutio kwa abiria wengi ndani ya jiji la Dar es salaam na mfano wa kuigwa kwa makondakta wenzake kwa namna ambavyo amekuwa akitoa huduma zake kwa kuchanganya sanaa ya ucheshi ndani ya kazi yake. Umaridadi wake kivazi na matumizi ya lugha safi pia ni miongoni m’a vile ambavyo vinaendelea kumuongezea sifa na kumpatia umaarufu si tu kwa abiria ambao anawahudumia kila siku bali hata kwa wafuasi wake kwenye mitandao ya kijamii Imezoeleka watoa huduma wengi kwenye daladala jiji Dar es salaam huvalia sare chufa za kazi au hata zilizochanika na wakati mwingine huzivaa nusu nusu juu ya nguo nyingine jambo ambao huonesha waziwazi kutokuipenda na kuithamini kazi yao. 📹 @eagansalla_gifted_sounds - - #bbcswahili #tanzania #ajira #foryoupagereels Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw