Skip to main content
Skip to main content

Uvamizi Wazee wa Agikuyu wakashifu polisi kwa uvamizi wa kanisa

  • | Citizen TV
    2,585 views
    Duration: 1:50
    Baraza la wazee wa jamii ya Agikuyu tawi la Nyeri, limemtaka inspekta jenerali wa Polisi Douglas Kanja, kuilainisha idara hiyo, kufuatia shambulizi la jumapili katika kanisa la ACK witima, linalodaiwa kutekelezwa na polisi. Wakizungumza saa chache baada ya baraza la makanisa nchini ,NCCK na tume ya kitaifa ya kutetea haki za kibinaadamu kutaka uwajibikaji Kutoka Kwa idara ya polisi, wazee hao wameelezea hofu ya mashambulizi zaidiea kushuhudiwa na kusababisha maafa, iwapo hatua kabambe hazitachukuliwa dhidi ya polisi waliowavamia waumini. Vile vile wamemtaka Rais William Ruto kukomesha cheche na matusi dhidi ya wapinzani wake, wakidai kuwa yanampunguzia uungwaji mkono, haswa eneo la mlima Kenya.