- 128 viewsMsemaji wa Serikali ya Tanzania, Greson Msigwa, amesema kuwa chanzo cha maji ni njia nafuu zaidi ya kuzalisha umeme kuliko vyanzo vingine, akibainisha kuwa gharama za uzalishaji wa umeme kwa kutumia maji ni shilingi 30 kwa uniti moja, huku kwa kutumia mitambo ya mafuta gharama zikiwa shilingi 940 kwa uniti moja. Alisisitiza kuwa licha ya kutumia gesi, ambayo imechangia katika uzalishaji wa umeme kwa gharama ya shilingi 170 kwa uniti, maji ni suluhisho la gharama nafuu kwa Watanzania. Msigwa ameeleza kuwa katika mwezi Disemba 2024, kiwango cha juu cha umeme kilifikia megawati 1900, na sasa wastani ni megawati 1880. Amesema bwawa la Mwalimu Nyerere linatoa matumaini makubwa katika kuongeza uzalishaji wa umeme. Aidha, amezungumzia miradi mikubwa ya kuboresha miundombinu ya umeme, ikiwemo mradi wa gridi imara wa zaidi ya shilingi trilioni 4, ambao umekamilika na kupunguza kelele za kukatika kwa umeme. Amebainisha kuwa Serikali inaendelea kujenga miradi ya usafirishaji wa umeme, kama vile njia ya Tanzania-Zambia, ambayo itasaidia kupeleka umeme kwenye nchi jirani. Pia, Msigwa alizungumzia miradi ya njia za kusafirisha umeme kutoka Chalinze hadi Dodoma, na mradi wa kuunganisha gridi ya taifa na nchi za Afrika Mashariki, ambapo Tanzania imefanikiwa kuunganisha na Kenya. Alisema mradi huu utakapokamilika, utawawezesha wateja wapya kupata umeme kutoka kwa gridi ya taifa. Ripoti ya Amri Ramadhani, VOA, Tanzania. #gresonmsigwa #msemaji #serikali #rufiji #mkoawapwani #bwawa #mwalimunyerere #gharama #serikali #voa #voaswahili #tanzania #gharamanafuu
'...uzalishaji wa umeme kwa kutumia maji ni shilingi 30 kwa uniti moja...'
- - Elimu bila mipaka ››
- 11 Aug 2025 - The British High Commissioner to Kenya, Neil Wigan is set to depart Kenya at the end of August marking an end to his 2 year tenure at the position.
- 11 Aug 2025 - Police in Eldoret have commenced investigations into an incident where a man received a parcel with three human fingers enclosed with six bullets.
- 11 Aug 2025 - Police in Eldoret have commenced investigations into an incident where a man received a parcel with three human fingers enclosed with six bullets.
- 11 Aug 2025 - Deputy Inspector General (DIG) of Police Eliud Lagat argues that the decision on whether to charge him over the death of blogger Albert Omondi Ojwang lies exclusively with the Director of Public Prosecutions (DPP) and not the courts.
- 11 Aug 2025 - The exposé contained footage allegedly showing minors being recruited into commercial sex work in Mai Mahiu
- 11 Aug 2025 - The ticketing malady witnessed in the ongoing CHAN 2024 competitions in Kenya has attracted censures from political leaders as many question the transparency of allowing football fans to secure tickets.
- 11 Aug 2025 - The clip of the assault went viral over the weekend.
- 11 Aug 2025 - "I am extremely sorry to be leaving Kenya after a whirlwind two years," Wigan said.
- 11 Aug 2025 - Several adverts have been posted online.
- 11 Aug 2025 - Mexico City's Benito Juarez International Airport suspended operations for several hours Sunday after heavy rains flooded the capital and caused poor visibility, authorities said.