Tukisalia kwenye masuala ya vifo vinavyotokana na kina mama kujifungua, visa hivyo vimeripotiwa kupungua katika hospitali mbalimbali kaunti ya kajiado baada ya wizara ya afya kaunti hiyo kupokea msaada wa mashine za picha.
Waziri wa afya kaunti ya kajiado, alex kilouwa, amesema msaada huo utasaidia kuimarisha huduma za uzazi kwenye hospitali mbalimbali zilizoko mashinani. Vifaa hivyo vya thamani ya shilingi milioni 50 vilitolewa na shirika la koica kutoka nchini korea kwa ushirikiano na kenya good neighbours.