Viongozi wa Kenya Kwanza kutoka eneo la bonde la ufa wamewahimiza wakazi kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi linaloendelea la uandikishaji wapiga kura linaloendeshwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka.
Wakizungumza katika Chuo cha Mafunzo ya kiufundi cha Kimasian wakati wa utoaji wa leseni za madereva kwa waendeshaji 146 wa bodaboda kutoka Kipkelion Mashariki, viongozi hao pia waliwataka waendeshaji bodaboda kusaidia zoezi hilo kwa kuwabeba wananchi wasioweza kufika katika vituo vya uandikishaji.
Kiongozi wa Wengi katika Seneti, Aaron Cheruiyot, aliwahimiza vijana waliofika umri wa miaka 18 kutuma maombi ya vitambulisho vya kitaifa.