- 9,257 viewsDuration: 2:50Iliwalazimu Wanasiasa wa upinzani kutafuta Kanisa mbadala kuhudhuria ibada ya Jumapili huko Meru, baada ya Naibu Rais Kithure Kindiki kufika Kanisani Methodist Kaaga, walikotarajiwa vinara hao kuhudhuria ibaada ya kutawazwa kwa askofu mpya wa jimbo hilo. Kabla ya kujumuika na waumini kwenye ibada hiyo, waandalizi wa upinzani walitimuliwa sehemu kulikoandaliwa shughuli hiyo, huku siasa za ubabe wa eneo hilo zikiendelea.