Viongozi wa makanisa wataka wahalifu kuondolewa katika dini

  • | Citizen TV
    117 views

    Viongozi wa makanisa wanasema matukio ya msitu wa Shakahola sio suala la Dini bali ni uhalifu. Viongozi hao waliofika mbele ya kamati maalum ya kuchunguza mauaji ya Shakahola, wanasema kuwa kuna haja ya kupiga msasa makanisa na wahubiri ili kuwaondoa wale ambao wanaendeleza madhehebu potovu na kutumia kanisa kuendeleza uhalifu. Kamati hiyo inajukumiwa kuchunguza kukithiri kwa makundi ya kidini na matukio yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 264.