Vurugu Murang’a: Polisi wakabiliana na wandani wa Gachagua

  • | Citizen TV
    5,679 views

    Viongozi wanaomuunga mkono aliyekuwa Naibu wa Rais Rigathi Gachagua leo walikabiliwa kwa risasi na vitoa machozi katika eneo la Kigumo kaunti ya Murang'a.Viongozi hao akiwemo Seneta Joe Nyutu wa Murang'a na mwenzake wa Nyandarua John Methu walikuwa wamehudhuria ibada katika kanisa la AIPCA Christ the King eneo la Kahuro kabla ya kuzuiliwa kufanya mkutano wa kisiasa. Kufuatia majibizano ya muda, polisi waliamua kukabiliana na viongozi hao. Magari ya viongozi hao pia yalipigwa mawe huku baadhi yakilengwa kwa risasi. Hii ni jumapili ya pili mfululizo kwa viongozi hao kukabiliwa na polisi. Haya yanajiri huku Gachagua anayeendelea na ziara yake nchini Marekani akiendelea kukosoa serikali ya ushirikiano kati ya Rais William Ruto na Raila Odinga.