Usimamizi wa idara ya polisi leo ulijipata mashakani wakati wa kikao na wabunge baada ya kufichuliwa kuwa licha ya maafisa wa polisi kukatwa pesa za bima, hazijakuwa zikifikishwa kwa kampuni za bima.kulingana na wabunge, kumekuwa na malalamishi kutoka kwa familia za polisi wanaofariki na kupata majeraha kazini wakisema wamekuwa wakifuata malipo ya fidia kwa zaidi ya miaka mitatu bila kupata hali inayozua wasiwasi. Pia masuali yaliibuka kuhusiana na baadhi ya miradi inayokwama na kutangazwa tena wakidai hii ni njama ya kufuja fedha za umma