Wadau kutoka kaunti sita wakutana mjini Kisii kuhusu kilimo cha kahawa

  • | Citizen TV
    144 views

    Wadau katika sekta ya ukuzaji kahawa kutoka kaunti 6 mkoa wa Nyanza wamekutana mjini Kisii kutathmini jinsi ya kuimarisha sekta hiyo. Wakizungumza maeneo ya Mosocho katika hafla hiyo iliyojumuisha shirika la wakulima -KPCU, Wakulima walihimizwa kuzidisha ukuzaji wa zao hilo kwani mpaka sasa ni asilimia 3 tu ya zao hilo inayosafirishwa hadi masoko ya ughaibuni.Waziri wa Kilimo wa kaunti ya Kisii, Dkt. Margeret Obara amesisitiza msimamo wake wa kufanikisha ukulima wa Kahawa na jinsi ya kukabili changamoto zilizopo.