Viongozi na wadau katika sekta ya elimu wameitaka serikali kuhakikisha kuwa kila mtoto anapata haki ya elimu ili kuwe na usawa katika jamii.
Wakizungumza wakati wa hafla ya kutoa basari kwa wanafunzi 400 kupitia Wakfu wa Hawkings Luvaga, washikadau hao wamesema kuwa bado kuna changamoto nyingi zinazokwamisha masomo kwa watoto wengi, huku wakiitaka serikali kuweka mikakati ya kuhakikisha elimu inatolewa bila malipo ili kuwafikia watoto wote. Aidha, machifu wametumia fursa hiyo kutoa onyo kali kwa wazazi watakaopatikana wakiwaacha watoto wao nyumbani badala ya kuwapeleka shuleni.