Wafugaji wa Isiolo wataka wafugaji kutoka Garissa kuondolewa

  • | Citizen TV
    265 views

    Takriban watu sita wameuwawa katika eneo la Garbatula kaunti ya Isiolo katika kipindi cha mwezi mmoja kufuatia mgogoro wa lishe. Wakizungumza kwenye kikao cha idara ya Usalama kilichoandaliwa katika eneo la Kinna, wazee wa eneo hilo wameeleza kusikitishwa na ujio wa wafugaji kutoka kaunti jirani ya Garissa wakati wa kiangazi kumesababisha mgogoro wa lishe kwa mifugo, hali ambayo ilepeleka vifo. Aidha wafugaji hao kutoka kaunti jirani wanaripotiwa kukita kambi eneo hilo, hali ambayo inachangia vita. Wafugaji sasa wanapigania ardhi na malisho.