- 1,180 viewsDuration: 2:36Huku kampeni za uchaguzi mdogo wa Chemundu-Kapngetuny zikiendelea kuchacha, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) katika Kaunti ya Nandi imewataka wagombea wote kuendesha kampeni zao kwa amani na kuheshimu sheria za uchaguzi. Mwenyekiti wa IEBC Nandi, Silas Rotich, amesema maandalizi ya uchaguzi huo yako katika hatua za mwisho, na mipango yote muhimu imewekwa tayari ili kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa uwazi na bila vurugu .Uchaguzi huo mdogo unaonekana kuwa wa ushindani mkali kati ya chama tawala cha United Democratic Alliance (UDA) na The Equitable Party, ambapo wagombea wa vyama hivyo viwili wamekuwa wakifanya kampeni za nguvu katika jitihada za kujinyakulia kura.