- 280 viewsDuration: 2:11Wahudumu wa bodaboda mjini Nanyuki wameandamana wakilalamikia Sheria ambazo zimewekwa na manispaa ya mji huo zinazowahitaji kupunguza kelele za bodaboda zao na kung'oa mataa yanayotoa mwangaza mkali. Wakiongea mjini Nanyuki baada ya kufanya maandamano ya amani wakielekea ofisi ya meneja wa manispaa, wanasema hawakuelimishwa kuhusu viwango vya kelele na pia ujumbe huu haukuwafikia kikamilifu kabla ya kutekelezwa kwa kipindi cha majuma mawili.