- 26 viewsWajane waliopoteza wake au waume zao katika Kaunti Ndogo ya Malindi wameitaka serikali kuwalinda kisheria wakisema kuwa ni miongoni mwa makundi yaliyotengwa humu nchini. Kundi hilo linasema linakabiliwa na changamoto nyingi katika jamii kama vile unyanyapaa, vitisho na unyanyasaji.Kulingana nao, wajane wana vyama zaidi ya 70 vya kujisaidia kupitia biashara ndogo eneo hilo ili kujikimu kimaisha. Sasa wanasisitiza kuwa kuna haja ya serikali kuwalinda.