- 50 viewsDuration: 2:16Wakaazi wa Malindi wamenufaika na matibabu ya bure kutoka kwa jamii ya Bohora mjini humo. Baadhi ya wakaazi wa Shella wamesema kambi hiyo ya matibabu imewasaidia pakubwa haswa watu wazima ambao wanaougua maradhi mbali mbali. Kwa mujibu wa daktari Adnan Mustafa aliyeongoza kikosi cha matabibu, baadhi ya watu waliohudumiwa waliguduliwa kuwa na ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu kwa mara ya kwanza baada ya kufanyiwa vipimo.