Skip to main content
Skip to main content

Wakaazi wa Rongai wataka ujenzi wa nyumba nafuu kusitishwa

  • | Citizen TV
    2,780 views
    Duration: 1:36
    Wakaazi wa Rongai katika eneo bunge la Kajiado Kaskazini, wanapinga ujenzi wa nyumba za bei nafuu katika ardhi ya Nakeel yenye ukubwa wa ekari 152. Wakazi hao wanasema mahakama iliamuru kusimamishwa kwa muda kwa mradi huo wa serikali , na kuendelezwa kwa shuguli za ujenzi kabla ya uamuzi kutolewa ni kinyume cha sheria. Wanasisitiza kuwa hawapingi maendeleo, lakini wanadai ardhi hiyo ilitengewa kuendeleza elimu inapasa kutumika kwa miradi kama vile ujenzi wa shule na taasisi za mafunzo. Sasa wanaitaka serikali kusitisha shughuli zote zinazoendelea hadi kesi hiyo itakaposikilizwa na kuamuliwa kikamilifu.