Wakazi wa Bori eneo bunge la Moyale kaunti ya Marsabit wameandamana kulalamikia kutengwa na serikali, huku eneo hilo likisalia nyuma kimaendeleo.
Wakazi hao wamenyoOshea kidole cha lawama serikali ya kaunti ya Marsabit kwa kutenga eneo hilo,hatua ambayo imewasababishia ukosefu wa maji,hospitali na miundo misingi bora. Wakazi wanalazimika kusafiri zaidi ya kilomita mia tatu kusaka huduma hizo muhimu. Vile vile swala tata la ukosefu wa mawimbi ya mawasiliano ni swala ambalo limezima matumaini ya wengi ya kujiendeleza kiuchumi.