- 555 viewsDuration: 3:41Wakazi wa eneo la Ilmunkush huko Kajiado East wanalalamikia kukosa umeme kwa zaidi ya miaka kumi licha ya nyaya na nguzo za stima kupitishiwa katika eneo hilo kitambo. Wanasema malalamishi yao kwa kampuni ya usambazaji umeme - Kenya Power, yanaendelea kupuuzwa. Na kama anavyoarifu Nancy Kering, hospitali katika eneo hilo zimekosa njia ya kuhifadhi dawa kutokana na ukosefu wa umeme.