Wakuu wa KEL Chemicals wadai kutishiwa na serikali

  • | Citizen TV
    1,392 views

    Wasimamizi wa kampuni ya kutengeneza mbolea ya KEL Chemicals sasa wanadai kuwa baadhi ya maafisa wakuu serikalini waliwalazimisha na kuwashinikiza kukiri kuwa walisambaza mbolea ghushi nchini. Afisa mkuu wa operesheni kwenye kampuni hiyo amesema kuwa alikamatwa na kuzuiliwa kwa muda baada ya mkutano uliohusisha wasimamizi wakuu serkalini kutibuka katika afisi ya rais. Aidha, maafisa wa kiwanda hicho ambao wamekana kwamba kampuni hiyo ilihusika na utengenezaji na usambazaji wa mbolea ghushi, wamedai kwamba kulikuwa na njama ya kulazimisha afisa mkuu wa kiwanda hicho kubeba lawama za sakata hiyo