- 320 viewsDuration: 2:06Walimu katika Kaunti ya Meru wametishia kususia kurejea shuleni baada ya likizo ya Aprili. Walimu hao wanatoa shinikizo kwa Tume ya Kuajiri Walimu (TSC) kushughulikia malalamishi yao, yakiwemo ajira ya kudumu kwa walimu wa sekondari msingi, malipo kwa walimu waliosahihisha mitihani ya KNEC Mwaka jana, Mfumo wa Afya wa SHA, pamoja na Uhuru wa kujisimamia kwa Sekondari msingi.