- 211 viewsDuration: 2:01Walimu Kutoka Kuria wametishia kususia na kujitenga na Muungano wa walimu KUPPET tawi la migori Kufuatia madai ya ubaguzi. Walimu hao wanasema wamejipata katika njia panda wanapopigania maslahi Yao katika kuppet Hali ambayo imelemaza utekelezaji wa makubaliano ya muungano huo wa walimu. Sasa wanasema kuwa watajitenga na shughuli za muungano huo hadi matakwa Yao yatakapotekelezwa. Walimu Kutoka Kuria wanalalamikia kutopata hata mwakilishi mmoja katika wadhifa wowote wa muungano huo wa KUPPET Hali ambayo wanaamini italemaza ushirikishwaji wao.