- 32 viewsWalimu wa shule za sekondari msingi kaunti ya samburu wamelalamikia kupuuzwa na mwajiri wao TSC kuhusiana na suala la ajira ya kudumu. Walimu hao ambao wametoa makataa ya wiki moja wanalalamikia kuhudumu katika mazingira magumu ya kazi wakilalamika kuwa mishahara wanayopokea ya shilingi elfu kumi na saba haikidhi mahitaji yao.