- 198 viewsDuration: 1:28Walimu katika kaunti ya Nyamira wanashinikiza ushirikiano mwema kati ya walimu, wanafunzi, jamii na serikali, ili kukuza mazingira mema shuleni haswa wakati wa mitihani ya kitaifa.walimu hao wameahidi kufanikisha uhusiano mwema na wanafunzi ili kuzuia mizozo inayosababisha kuchomwa kwa shule na uharibifu wa mali. Aidha walimu hao wameomba kuimarishwa kwa miundo msingi shuleni, na haki za walimu kuzingatiwa wanapopandishwa vyeo ili kuwapa motisha kazini.